Pakistan inazuwia helikopta ya India

Msemaji wa jeshi la Pakistan, amesema kuwa helikopta ya jeshi la India imelazimishwa kutua baada ya kuingia katika anga ya Pakistan hii leo.

Haki miliki ya picha AP

Maafisa wane wa usalama wa India waliowekwa kizuizini sasa wameachiliwa huru.

Haijulikani vipi helikopta hiyo ilivuka mpaka baina ya nchi mbili hizo katika eneo la Skardu, kaskazini mwa Pakistan.

Inafikiriwa hali mbaya ya hewa ilichangia.