Libya yasherehekea ukombozi

Walibya wanapepea bendera za serikali mpya Haki miliki ya picha Reuters

Wakuu wa Libya wametangaza rasmi ukombozi wa nchi katika sherehe iliyofanywa Benghazi, nje ya kambi ambako uasi dhidi ya Kanali Gaddafi ulianza mwezi wa Februari.

Kiongozi wa serikali ya mpito, Mustafa Abdel Jalil alisujudu kumshukuru Mungu kwa ushindi wao, huku umati ukishangilia.

Aliwasihi watu wasameheane, wapatane, na kuwa na umoja.

Aliwashukuru wote walioshiriki katika mapinduzi - kutoka wapiganaji hadi wafanya biashara na waandishi wa habari waliowaunga mkono.

Alisema Libya itachukua sharia za Kiislamu kama msingi wake.

Na alizitakia Syria na Yemen mafanikio katika maandamano yao dhidi ya serikali.

Bado hakuna uhakika viongozi wepya wa Libya wataifanya nini maiti ya Kanali Gaddafi.

Kuna taarifa kutoka serikali ya mpito kwamba imeamuliwa kuwa maiti itakabidhiwa kwa jamaa zake.

Lakini taarifa nyengine zinaonesha huo siyo uamuzi wa mwisho.