Mlipuko mwingine watokea mjini Nairobi

Taarifa kutoka Kenya zinasema kumetokea mlipuko mwingine katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.

Polisi wanasema mtu mmoja ameuawa na wengine kumi na wawili wamejeruhiwa.

Mlipuko huo umetokea kwenye kituo cha basi. Kamishna wa Polisi Mathew Iteere amesema shambulio hilo halina uhusiano na shambulio lilitokea kwenye baa Jumatatu.

Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu,"majeruhi wanane wamekimbizwa hospital ya Taifa ya Kenyatta, na mmoja amekufa baada ya mlipuko," Shirika hilo limesema kupitia mtandao wa jamii wa Twitter.

Shambulio hilo linatokea huku Ubalozi wa Marekani nchini Kenya ukiwa umeonya kuwa mashambulio yangetokea, wakati taifa hilo linapigana na wapiganaji wa Kiislam katika nchi jirani ya Somalia.

Taarafa kamili bado zinakuja,

Taarifa hizi zinakuja wakati shambulio lingine lilitokea mapema Jumatatu katika baa moja mjini Nairobi.

Watu kumi na watatu wanawalijeruhiwa wakati gurunedi lilipotupwa kwenye chumba.

Wasiwasi uliibuka kuwa kundi la al-Shabaab lilihusika, lakini mamlaka zinasema hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa wanahusika.