Cameroon yamfukuza kocha wake

Clemente Haki miliki ya picha Getty
Image caption Clemente afukuzwa kazi

Cameroon imemfukuza kazi kocha wake Javier Clemente huku kocha huyo akiwa bado amesaliwa na miezi minane katika mkataba wake.

Chama cha soka cha Cameroon kimethibitisha kumuachisha kazi siku ya Jumanne, na kumaliza wiki akdhaa za tetesi kuhusiana na hatma ya kocha huyo kutoka Uhispania.

Kocha huyo alikuwepo wakati Simba hao waliposhindwa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2012, jambo lililoshangaza wengi.

"Clemente na wasaidizi wake waliambiwa kuwa wameachishwa kazi jana," amesema katibu mkuu wa chama cha soka cha Cameroon Sidiki Tombi.

Mfaransa Denis Lavagne, ambaye ni kocha wa klabu bingwa ya Cameroon Coton Sport, anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo.