Vijana wa ANC wadai mabadiliko

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandamanaji mjini Johannesburg

Waandamanaji wapatao elfu saba Afrika Kusini katika mji mkuu Johannesburg wamedai kuwepo nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi kwa watu weusi.

Waandamanaji hai walipunga mabango yao wakitaka migodi itaifishwe ili kupunguza ushawishi wa wazungu wanaomiliki biashara nchini humo.

Jumuiya ya Vijana ya Chama kinachotawala iliandaa iliandaa maandamano yakiwa na maudhui ‘uhuru wa kiuchumi ni wa maisha yetu’

Utawala wa weupe wachache (ubaguzi wa rangi) ulimalizika Afrika Kusini mwaka 1994.

Serikali ya Chama tawala cha ANC imekuwa ikipambana na kuongezeka kwa umaskini na kuosefu wa ajira baada ya kuongoza miongo mingi ya kupambana na ubaguzi wa rangi ambao uliwabagua watu weusi.

Waziri wa Elimu ya Juu Blade Nzmande amesema Alhamis kuwa tatizo la ajira Afrika Kusini linafikia kiasi 40% na ni kubwa miongoni mwa vijana.

Shule kadhaa za weusi kwenye viunga vya Johannesburg hazikuwa na wanafunzi wengi wakiwa wamejiunga kwenye maandamano hayo kuelekea Makao Makuu ya Soko la Hisa na Madini, shirika la habari la SAPA.

Waandamanaji walikuwa wakiimba ‘ua kaburu’ (Kiafrikana) kinyume na agizo la mahakama kuuzuia wimbo huo kuwa unachochea chuki za kibaguzi.