Ulaya yaomba mkopo kutoka Uchina

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Klaus Regling: anaongoza jitihada za Ulaya kupata mkopo Uchina

Kiongozi wa hazina ya mkopo wa dhamana katika mataifa ya Ulaya yanayotumia sarafu ya Euro Klaus Regling amewasili mjini Beijing,Uchina katika harakati za kuishawishi Uchina kuwekeza fedha katika hazina hiyo.

Fedha hizo zitatumika kuzisaidia nchi wanachama wanaokabiliwa na tatizo la madeni.

Mwandishi wa BBC mjini Beijing anaamini kwamba Uchina huenda ikaridhia ombi hili na kuwekeza dola bilioni mia moja katika hazina hiyo. Hata hivyo Uchina imesisitiza kwamba lazima ihakikishiwe kuwa fedha hizi zitalindwa kabisa.

Viongozi wa mataifa hayo ya Ulaya tayari wameafikiana kuongeza hazina hiyo kwa dola trilioni moja nukta nne.