Mapigano yazuka Sudan Kusini

Kikundi kikubwa cha wapiganaji wa Sudan Kusini, kimeshambulia mji katika jimbo la Unity lenye mafuta mengi, na kuuwa watu kama 15.

Haki miliki ya picha

Haijulikani kama wapiganaji hao sasa wanaudhibiti mji wa Mayom.

Hapo jana wapiganaji wa Jeshi la Ukombozi wa Sudan Kusini, SSLA, waliwaonya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada kuondoka katika jimbo la Unity.

Na sasa wanatishia jimbo la jirani la Warrup.