Mkuu wa asifu kazi NATO Libya

Haki miliki ya picha Reuters (audio)
Image caption Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen

Mkuu wa Nato Anders Fogh Rasmussen amesema majeshi yake yamefanya kazi nzuri kusaidia Libya wakati wa mapinduzi ya kiraia dhidi ya marehemu Kanali Muammar Gaddafi.

Bw Rasmussen yuko Tripoli kuhitimisha rasmi ujumbe wa NATO nchini lIbya.

Amesema Nato ingeweza kusaidia utawala mpya wa Libya kwa ulinzi na mageuzi kuelekea demokrasia iwapo wangeombwa.

Vikosi vya Nato vikifanya kazi chini ya amri ya Baraza la Umoja wa Mataifa kuwalinda raia ilianza harakati zake mwezi Machi wakati vikosi vya Gaddafi vilipoamua kupambana na waandamanaji.

Ujumbe wa Nato unkamilisha rasmi kazi zake Libya saa dakika moja kabla ya kuingia saa sita usiku kwa saa za Libya (21:59 GMT) Jumatatu.

Bw. Rasmussen amesema wamefanya mazungumzo na viongozi wa NTC akiwemo mwenyekiti Mustafa Abdul Jalil, kuhusu hatma y Libya katika siku zijazo na mwelekeo wa mageuzi ya kidemokrasia

"Mmechukua hatua kubadilisha historia na hatma yenu. Nasi tumewalinda. Pamoja tumefanikiwa. Libya hatimaye iko huru, kuanzia Benghazi to Brega Brega, mpaka Misrata hadi kwenue milima ya Nafusa na Tripoli.

"Nchi nyingi za Kiarabu watatufahamu na kutuamini, wengi walifanya kazi pamoja kuwalinda ninyi. Ni matumaini yangu kuwa Libya yenye uhuru, demokrasia itajiunga nasi kama washirika siku moja lakini hilo ni uamuzi wenye. Hatma ya Libya sasa iko mikononi mwenu.

Bw Jalil alitoa shukrani zake kwa msaada kutoka NATO na nchi nyingine za kigeni pamoja na vikosi vya Libya.

Mapema Bw Rasmussen alisema Nato ingeweza kusaidia ‘mageuzi ya ulinzi na usalama’ lakini sasa ilikuwa ni wakati kwa Umoja wa Mataifa kusaidia Libya.

Aliongeza kuwa harakati za NATO zimeiunganisha Libya na kuwa ‘mojawapo ya kazi ya kihistoria ya NATO iliyofanikiwa.