Mtoto India awa wa bilioni saba duniani

Haki miliki ya picha online
Image caption Mtoto Nargis awa mtu wa bilioni saba duniani

Mtoto aliyezaliwa nchini India ametangazwa na shirika linalotetea haki za watoto la Plan International kuwa mtu wa bilioni saba.

Mtoto Nargis alizaliwa saa kumi na moja kasoro dakika tano (saa za Afrika Mashariki) katika kijiji cha Mall katika jimbo la Uttar Pradesh nchini Libya.

Plan International linasema Nargis amechaguliwa kama ishara kwa sababu si rahisi kujua kihalisi kuzaliwa kwa mtoto wa bilioni saba.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa Jumatatu 31 Octoba, idadi ya watu duniani itafikia bilioni saba.

Mapema Jumatatu, Ufilipino ilitangaza mtoto wake wa bilioni saba, mtoto wa kike aliyezaliwa katika hospitali ya Manila.

Kila dakika watoto 51 wanazaliwa India, 11 kati yao ni kutoka jimbo lenye watu watu wengi la Uttar Pradesh.

Nargis alizaliwa na wazazi Vinita na Ajay Kumar Jumatatu katika hospitali ya serikali kijijini Mall karibu kilometa 50 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo Lucknow, afisa mmoja wa Plan International ameiambia BBC.

Mtoto huyo Nargis wa mkulima maskini alichaguliwa kuwa wa bilioni saba kuelekeza malengo yake ya kupambana na utamaduni potofu dhidi ya watoto wa kike na idadi yao, shirika hilo limesema.

Mamia kwa maelfu ya mimba changa za watoto wa kike zinatolewa nchini Inida kila mwaka, licha ya haki ya kujua jinsia ya mtoto na matumizi ya teknolojia ya mionzi kujua jinsia kuzuiliwa kisheria.

Picha za mtoto Nargis zilionyeshwa katika hafla iliyohudhuriwa na karibu wanakijiji 250 katika hospitali hiyo, mwandishi wa BBC Ram Dutt Tripathi amearifu kutoka Mall.

Maafisa wa afya walitoa cheti cha kuzaliwa kwa baba wa mtoto katika maadhimisho hayo.

"Tunamuombea mtoto wetu ," Ajay Kumar alisema. "Huyu ni Lakshmi [mungu wa utajiri wa kihindu], ataleta bahati nzuri kwetu," alisema.

Hata hivyo katika Urussi ambayo ni miongoni mwa nchi chache ambazo idadi ya wakaazi wake inazidi kupungua--watoto watatu waliozaliwa Jumaatatu usiku wamepewa vyeti vya kuwatambulisha kuwa ni mtu wa billioni 7 duniani. .

Mmojawao alizaliwa Petropavlovsk-Kamchatsky, Mashariki ya Mbali, na wengine katika miji ya Kaliningrad na St Petersburg. Umoja wa Mataifa umefahamisha wazi kwamba vyeti hivi ni ishara tu na hazina uzito nje ya Urussi.

Hata hivyo kuzaliwa kwa watoto hao kumetangazwa kwa marefu na mapana nchini Urussi kupitia wavuti wa Rais. Katika Kamchatsky inafahamika baada ya mwaka mmoja mama wa mtoto billioni 7 atatunukiwa fleti ya vyumba viwili .

Kinyume na kuzaliwa kwa mtoto billioni 6 mnamo mwaka 1999;safari hii Umoja wa Mataifa hautamtambua rasmi mtoto mmoja na mahali alikozaliwa. Umoja wa Mataifa unasema kuzaliwa kwa mtu wa billioni 7 si wakati wa kusherehekea,lakini ni wa kutafakari mustkbala wa dunia yetu.

.