Huwezi kusikiliza tena

Utalii watikisika Kenya

Utalii ni moja ya sekta muhimu sana nchini Kenya.

Matukio ya utekaji nyara ya raia wa kigeni yaliyotokea hivi karibuni hasa katika pwani ya Kenya, ikiwemo Lamu yametikisa sekta hiyo ya utalii na usalama wa raia wa Kenya kwa ujumla.

Utekaji huo unaodhaniwa kufanywa na kundi la al-Shabab nchini Somalia umesababisha nchi ya Kenya kuingia na kupambana nao kwa minajil ya kulinda raia wake na uchumi pia.

Kutaka kufahamu namna sekta hiyo iliyoathirika, mwandishi wetu Zuhura Yunus alizungumza na waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala mwanzo akielezea kwanini Kenya ilichukua uamuzi wa kuingia Somalia