Huwezi kusikiliza tena

Sarafu ya euro yaiyumbisha Ulaya

Kwa muda sasa dunia imeshuhudia mgogoro kwa nchi zinazotumia sarafu ya Euro ambapo kuna wakati kulikuwa na tishio mataifa ya Ulaya yanayotumia sarafu ya Euro yangesambaratika, hali bado haijaimarika.

Katika mjadala huu tunazungumzia kuyumba kwa uchumi wa mataifa yanayotumia sarafu ya euro, nchi zetu za Afrika hasa Mashariki na Kati zinaathirika kwa kiasi gani, tuna wasiwasi au serikali zetu hazikoseshwi usingizi na yanayotokea barani Ulaya na kuna funzo lolote tunalolipata?

Utaratibu uliotumika safari hii ni tofauti ambapo msikilizaji alipewa fursa ya kumwuuliza maswali mtaalam wa uchumi, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye kwa sasa yupo Marekani.

Aliyeuendesha mjadala huu ni Charles Hilary