Rwanda yaangamiza silaha

Maafisa nchini Rwanda wameangamiza tani kadhaa za silaha.

Hiyo ni sehemu ya mikakati ya kupunguza silaha zilizo mikononi mwa raia ili kudumisha usalama wa nchi.

Silaha zaidi zitaangamizwa katika siku za hivi karibuni.

Rwanda inasema baadhi ya silaha zilipatikana kutoka kwa wapiganaji wa zamani na raia.

Rwanda imekuwa ikihusika katika vita vya Congo, kaskazini mwa nchi hiyo, kwa miaka kadha.