Kanisa lashambuliwa Garissa, Kenya

Wanajeshi wa Kenya Haki miliki ya picha Reuters

Shambulio la guruneti kwenye kanisa moja mjini Garisa, kaskazini mashariki mwa Kenya, limewauwa watu wawili na wengine wawili kujeruhiwa.

Mwandishi wa BBC mjini humo anasema, shambulio hilo lilitokea usiku, na hadi sasa haijulikani wahusika, wala lengo lao la kushambulia kanisa hilo.

Vikosi vya usalama vimeanza uchunguzi, na mamia ya polisi wanaoenekana wakishika doria mjini humo.

Kumefanywa mashambulio ya maguruneti ya hapa na pale nchini Kenya, tangu jeshi lake kuingia nchini Somalia, ili kuwasaka wapiganaji wa kikundi cha Al-Shabab kusini mwa Somalia.