Bingwa wa ndondi Frazier afariki

Mwanandondi Joe Frazier Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanandondi Joe Frazier

Aliyekuwa bingwa wa dunia wa ndondi wa uzani wa juu, Joe Frazier amefariki dunia.

Frazier, mwenye umri wa miaka 67 aligunduliwa kuwa na maradhi ya saratani wiki tatu zilizopita.

Frazier maarufu sana kama Smokin Joe alikuwa mwenye umbo mdogo lakini alikuwa mkali sana katika masumbwi. Alikuwa mwanandondi wa kwanza kumshinda bingwa Muhammad Ali, kwa pigo la ushindi katika mchuano wao mkali uliodumu raundi kumi na tano katika ukumbi wa madison square mnamo mwaka 1971.

Hata hivyo alishindwa kuandikisha ushindi wowote dhidi ya Ali katika michuano yao miwili iliyofuatia na kwa miaka mingi alijawa na hasira kwa kushindwa kumpiku Ali.

Joe Frazier alipata ushindi wa dunia katika uzani wa juu mwaka 1970 kwa kumshinda Jimmy Ellis.

Alitetea taji lake mara nne kabla ya kushindwa na George Foreman mwaka 1973.