Oxfam yaondoka mpakani Sudan

Shirika la msaada la Uingereza, Oxfam, linawahamisha wafanyakazi wake kutoka eneo la mpakani lenye mzozo la Sudan Kusini, kwa sababu ya ghasia zinazozidi.

Haki miliki ya picha AFP

Oxfam inasema wafanyakazi wake wamearifu kwamba ndege na mizinga imetumiwa kufanya mashambulio ya saa kadha siku ya Ijumaa, katika jimbo la Upper Nile.

Shirika hilo linasema kuwa maelfu ya wakimbizi wanaendelea kuvuka mpaka na kutoka kaskazini wakihitaji chakula, maji na hifadhi.

Uamuzi huo umetangazwa siku moja baada ya mkuu wa shughuli za kuweka amani za Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous, kusema kuwa mvutano unaozidi mpakani unatishia kugeuka vita kamili baina ya Sudan Kaskazini na taifa jirani, taifa jipya, la Sudan Kusini.