Kura ya maoni yafanywa Equatorial Guinea

Upigaji kura unaendelea Equatorial Guinea, katika kura ya maoni juu ya mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa na Rais Teodoro Obiang Nguema, ambaye ameongoza nchi kwa zaidi ya miaka 30.

Haki miliki ya picha AP

Katiba hiyo inapendekeza kuwa rais atumike kwa mihula miwili tu, na itaunda wadhifa mpya wa makamo wa rais.

Wanaharakati wa haki za kibinaadamu na upinzani nchini Equatorial Guinea, wanasema mabadailiko hayo hayana maana, na yataendeleza madaraka ya rais, ambaye ataweza kumteua mtu atayemrithi.