Upinzani wakataa kura ya maoni

Haki miliki ya picha equatorial guinea
Image caption Rais wa Equetorial Guinea Teodoro Obiang Nguema

Upinzani nchini Equatorial Guinea kimetupilia mbali matokeo ya kura ya maoni inayohusu mabadiliko ya katiba yanayoweka ukomo kwa awamu mbili za Urais na kuita udanganyifu katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.

Pablo Mba Nsang wa chama cha Convergence for Social Democracy Party ameiambia BBC kuwa ni njia ya kufanya akae madarakani kwa miaka 14 mingine.

Serikali inasema kuwa kwa zaidi ya kura 3/5 ya kura zote zilizopigwa asilimia 90 ya kura wameunga mkono kura ya maoni.

Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo amekuwa madarakani kwa miaka 32.

Haijafahamika iwapo Rais Obiang, Rais aliyekaa madakarani kwa muda mrefu zaidi barani kama ataachia madaraka yake katika mwishoni mwa muhula wake 2016, shirika la habari la AFP.

Wakosoaji wanasema mabadiliko ya katiba yanayohusisha kuwepo kwa nafasi ya makamu wa Rais yanamruhusu yeye kuteua mrithi wake.

"Kuna wasiwasi wa wazi hapa kuwa mtoto wake mkubwa Teodoro anaandaliwa kuwa Rais ajaye wa nchi hiyo” Joseph Kraus, anayefanya kazi na kundi la kutetea haki za Binadamu lenye makao yake makuu Washington la Equatorial Guinea Justice, amekiambia kipindi cha BBC World Today.

Teodoro Nguema Obiang Mangue, ambaye kwa sasa ni waziri wa kilimo anashutumiwa kwa kutumia nafasi yake na Rais wa baba yake kukwapua utajiri wanchi hiyo.

Mwezi uliopita serikali ya Marekani ilisema ingechukua mali yenye thamani ya $ 70 milioni (£44m) anayoimiliki.