Papa Benedikte wa16 kuzuru Benin

Pope Benedicte Haki miliki ya picha Reuters

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict wa XVI anatarajiwa kuzuru nchini Benin ikiwa ni ziara yake ya pili barani Afrika.

Makao Makuu ya Vatican yanasema Papa analeta ujumbe wa amani na maridhiano kwa Waafrika.

Kuchaguliwa kwa taifa hili kama mwenyeji wa ziara ya Papa Afrika pia kuna umuhimu wake. Kwanza Benin ndiyo aliyoathirika zaidi na biashara ya utumwa ambapo raia wengi waliuzwa kama watumwa katika nchi za magharibi. Kanisa Katoliki limeomba mshamaha kwa taifa hili katika ziara ya awali za papa hayati Yohana wa Pili.

Aidha mwaka huu Benin inaadhimisha karne moja na nusu tangu kuitikia wito wa Ukristo ambapo taifa hilo lilitoa askofu wa kwanza mweusi kwa Vatican.Kadinali Bernadin Gantin amekuwa mwanachama wa baraza kuu la makadinali huko Vatican maarufu kama Curia na ambalo huwa na jukumu la kumteuwa Papa Mpya.

Raia huyo Benin ambeya sasa ni marehemu amewahi kuwa amekuwa mkuu wa makadinali hadi mwaka 2004 ambapo papa wa sasa Benedite 16 alichukua nafasi hiyo wakati huo akijulikana kama kadinali Joseph Ratzinger.

Hayati Papa Yohana Paulo wa pili aliwahi kuzuru Benin miaka ya 1982 na 1993 na hii itakua ziara ya tatu taifa hili kumpokea kiongozi wa kanisa katoliki duniani.

Akiwa Benin Papa Benedikte wa 16 atatembelea kaburi la Kadinali na rafiki wake Berndin Gantin ,katika mji wa Ouidah, ambapo wamishonari wa kwanza walifika mwaka 1861. Benin ilikuwa kitovu cha imani ya kikiristo na kusambaa kwake katika nchi jirani za Togo, Ghana na Nigeria.

Japo raia wake wameendelea kushikilia imani za kitamaduni hususan Vodoo asili mia 30 ya raia wa Benin ni waumini wa katoliki, huku wengine wakifuata Uisilamu na imani za Kilokole.