Askofu Tutu alaani muswada wa Habari

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Askofu Mkuu Desmond Tutu ashutumu vikali muswada wa habari Afrika Kusini

Bunge la Afrika Kusini linapigia kura muswada wa habari wenye utata.

Muswada huo ulisababisha maandamano katika miji mikubwa kadhaa ya nchi hiyo.

Wanaoupinga wanasema sheria hiyo inatishia uhuru wa kujieleza na ni kinyume na katiba.

Askofu mkuu Desmond Tutu ameielezea sheria hiyo kuwa si haki na ni fedheha kwa Waafrika Kusini.

Chama kinachotawala ANC kinasema muswada huo unahitajika kwa ajili ya usalama wa Taifa.

Askofu Mkuu Tutu ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ameshutumu vikali sheria hiyo mpya inayodhibiti vyombo vya habari.

Ameuita ‘unaofedhehesha’ na kuonya kuwa unaweza kutumika kudhibiti ‘wapiga mbiu na uandishi wa habari za uchunguzi.’

Waandishi wa habari wa Afrika Kusini wakiwa wamevaa nguo nyeusi wameandamana kupinga kile walichokiita ‘muswada wa siri’ nje ya makao makuu ya chama tawala ANC.

Chama hicho African National Congress kina theluthi mbili ya wingi wa wabunge na kufanya muswada huo kupita.

Muswada wa Kulinda taarifa za Taifa unapendekeza hatua kali kwa yeyote anayekutwa na nyaraka za siri za serikali.

Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko mjini Johannesburg anasema muswada huo unatazamwa wakati huu baada ya msemaji wa Rais Jacob Zuma, Mac Maharaj kufungua mashtaka dhidi ya gazeti la Mail na Guardian- kuzuia habari zinazomhusisha na mkataba wa silaha wenye utata mwaka 1999 zisiandikwe.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliandika habari hiyo kwa kutumia nyaraka za siri za serikali lakini katika sheria hii mpya waandishi na wahariri wao watakabiliwa na adhabu ya kifungo jela kwa kosa kama hilo, anasema.

  • Unaipa serikali mamlaka ya kuzipa usiri nyaraka zake kwa 'maslahi ya Taifa'
  • "Maslahi ya Taifa " ina maana pana, wakosoaji wanasema, na inaweza kuhusisha taarifa za serikali zenye ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu
  • Kifungo cha hadi miaka 25 jela kwa mtu atakayekutwa na nyaraka za siri au analiyehifadhi siri za serikali
  • Hakuna kifungu cha maslahi ya Taifa
  • Wananchi na waandishi wa habari kuchukuliwa kama makachero wa kigeni iwapo watakutwa na taarifa zenye mwelekeo wa siri za Taifa.

Askofu Mkuu Tutu alisema ‘ni kuwatukana waafrika Kusini wote kwa muswada wa sheria ya tumbo ambayo inawazuia wapiga mbiu na uandishi wa habari za uchunguzi…na hilo linafanya Taifa kuwajibika kwa taifa peke yake."

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kuhusu uandishi Nadine Gordimer kutoka Afrika Kusini pia amelaani muswada huo, ambaye aliongeza kuwa unairudisha nyuma nchi hiyo wakati wa utawala wa weupe wachache, kituo cha habari cha Johannesburg cha Times Live kimeripoti.

Alisema, ‘muswada uko kinyume kabisa’ na uhuru, alisema.

"Vitendo vya rushwa na upendeleo ambavyo wanasiasa wanavifanya vinawaweka bayana iwapo kama tuna uhuru wa kujieleza," Bi Gordimer alinukuliwa akisema.

Klabu ya waandishi wa Habari Afrika Kusini (NPC) – kimeunga mkono kampeni ‘haki ya kujua’ inayoendeshwa na kudni moja, na ktoa wito kwa watu kuvaa nguo nyeusi na kiita siku hiyo ya kupigia kura muswada huo "Black Tuesday" kurejea udhibiti wa vyombo vya habari enzi za ubaguzi wa rangi.