Mkuu wa tume ya ufisadi afukuzwa Nigeria

Image caption Bi Farida Waziri

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amemfukuza kazi mkuu wa taasisi ya kupinga rushwa nchini humo, Tume ya Uhalifu wa Uchumi na Fedha (EFCC).

Hakuna sababu zozote zilizotolewa na ofisi ya rais ya kutolewa kwa Farida Waziri.

Aliyekuwa kabla yake huko EFCC, Nuhu Ribadu, alitolewa katikati ya muda wake mwaka 2007 muda mfupi baada ya Umaru Yar'Adua kuwa rais.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakiikosoa taasisi hiyo, wakiishutumu kushawishiwa na wanasiasa.

Nigeria imekuwa ikigubikwa na madai kuwa utajiri wake umekuwa ukitumika kwa ufisadi tangu kuanza kwa ongezeko la uzalishaji wa mafuta miaka ya 70.

Naibu wa Bi Waziri, Ibrahim Lamorde, ameteuliwa na rais kuongoza taasisi hiyo.

'Kesi kulingana na vichwa vya habari'

Msemaji wa EFCC Femi Babafemi ameliambia shirika la habari la AP kuwa Bi Waziri alikuwa bado na mwaka mmoja kuitumikia taasisi hiyo.

EFCC iliundwa mwaka 2002, miaka mitatau baada ya kumalizika kwa utawala wa kijeshi Nigeria.

Mwandishi wa BBC Jonah Fisher mjini Lagos alisema hadhi yake inachukuliwa na watu kwa hisia tofauti.

Kwa wakati huo, iliwashtaki wanasiasa 30, ambapo wanne tu walitiwa hatiani na hamna hata mmoja kwa sasa aliye gerezani.

Baadhi wamesema imewachagua kwa maana yao kwa minajil ya kisiasa zaidi.

Mwezi Agosti, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lilisema mfumo wa kisiasa wa Nigeria ni sababu ya kushindwa kwa EFCC ambayo imeendelea "kumzawadia mtu badala ya kupambana na rushwa".

Mwandishi wetu alisema wakosoaji wa Bi Waziri wanaamini tume hiyo imepoteza nguvu wakati alipokuwa madarakani na badala ya kutumia mahakama alikuwa "akihukumu kulingana na vichwa vya habari".

Amesema baadhi wamediriki hata kumshutumu kwa ufisadi- madai ambayo maisha amekuwa akikana.