Muuaji wa Norway hana akili timamu

Madaktari wa magonjwa ya akili wamekubaliana kuwa mtu aliyeua watu 77 mwezi Julai alikuwa na matatizo ya akili alipofanya uhalifu huo.

Wameona kuwa Anders Behring Breivik alikuwa hana akili timamu, aliamini alichaguliwa kuokoa watu wa Norway, na kuamua nani aishi na nani afe.

Bado atashtakiwa mwezi Aprili kwa kuweka bomu mjini Oslo na kuwapiga risasi na kuua idadi kubwa ya watu katika kisiwa cha Utoeya.

Hata hivyo, uwezekano mkubwa ni kuwa atapelekwa kwenye taasisi ya wagonjwa wa akili badala ya gerezani.