Muswada tata wapitishwa Afrika Kusini

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Chama cha ANC kiliunga mkono muswada huo tata

Bunge la Afrika Kusini limepitisha kwa kura nyingi muswada wa sheria tata kuhusu kulinda siri za serikali ambao umesababisha maandamano katika miji kadhaa nchini humo.

Wapinzani wa muswada huo wanasema sheria hiyo mpya inayopendekezwa inatishia usalama wa kujieleza na inakiuka katiba.

Askofu Mkuu Desmond Tutu ameielezea sheria hiyo kuwa haifai na ni matusi kwa wananchi wa Afrika Kusini.

Hata hivyo chama tawala cha African National Congress, ANC, kimesisitiza kuwa sheria hiyo inahitajika kulinda usalama wa taifa.

Muswada huo bado unahitaji kupitishwa na baraza la juu la bunge na Rais Jacob Zuma ili kuwa sheria.