ECOWAS yagomea uchaguzi Gambia

Haki miliki ya picha online
Image caption Rais Yahya Jammeh wa Gambia

Gambia haina mazingira mazuri ya kisiasa ya kufanya uchaguzi wa Urais uwe huru na wa haki, taasisi ya ECOWAS imesema.

Ecowas limesema kwa sababu hiyo haitatuma waangalizi wake kwenye uchaguzi unaofanyika Alhamis.

Ujumbe wake wa awali kufanya uchunguzi wa mazingira ya uchaguzi huo ulikuta kuna ukandamizaji na kiwango cha juu kisichokubalika wa vyombo vya habari kunakofanywa na chama tawala.

Rais Yahya Jammeh alichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwaka 1994 na akashinda uchaguzi mara tatu huku kukiwa na shutuma nyingi tangu wakati huo.

Amekuwa akituhumiwa kwa kutovumilia upinzani na kutokuwa na makubaliano katika nchi niyo ndogo ya Afrika Magharibi inayosifika kwa utalii.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mustapha Carayol, amekasirishwa na uamuzi wa Ecowas.

"Tuhuma zote hizo ni uongo," ameiambia BBC.

Bw Jammeh, 46, anachuana na Ousainou Darboe, kiongozi wa chama cha United Democratic na Hamat Bah, anayeungwa mkono na muungano wa vyama vya upinzani.

"Maandalizi na mazingira ya kisiasa kwa hicho kinachoitwa uchaguzi tayari umeshaamuliwa na tume kutokuwa huru sawa na haki," Jumuiya ya ECOWAS yenye wanachama 15 imesema katika taarifa yake.

Imesema uchunguzi wak uligundua kuwa "upinzani na wapiga kura umegubikwa na ukandamizaji na uonevu."

Kabla ya uchaguzi wa 2006, Ecowas ilitoa wito kwa wapinzani kutosusia uchaguzi na kuhatarisha "mchakato wa demokrasia ya nchi".

Serikali ya Bw Jammeh umekosolewa na makundi ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu kwa mwelekeo wake wa kuzima uhuru wa raia hasa uhuru wa kujieleza.

Mwandishi wa BBC anasema kuna mabango machache ya upinzani nchini humo..

Mabango makubwa yanaonekana katika mji mkuu Banjul, yakisomeka kuwa Bw Jammeh ni "fundi wa kutengeneza amani na mshindi n mjenzi wa Taifa ", Shirika la AFP linaripoti.