NATO yauwa Wapakistan

Waziri Mkuu wa Pakistan, Yousef Raza Gilani, ameelezea shambulio la ndege za NATO dhidi ya kituo cha ukaguzi cha Pakistan kuwa shambulio dhidi ya umoja na uhuru wa Pakistan.

Haki miliki ya picha AFP

Wanajeshi 25 wa Pakistan waliuwawa katika shambulio hilo karibu na mpaka wa Afghanistan.

Bwana Gilani alisema Pakistan imeungana na haitoruhusu mtu yeyote kuishambulia.

Bwana Gilani alikuwa anakwenda Islamabad kwa mkutano wa dharura kuhusu ulinzi, kujadili tukio hilo.

Jeshi limesema lina haki ya kulipiza kisasi.

NATO inasema inachunguza tukio hilo kujua ukweli.