Rais Saleh hana madaraka Yemen

Siku moja baada ya kutangazwa uchaguzi wa kumuondoa madarakani, Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen, ametangaza msamaha wa jumla kwa wafungwa.

Haki miliki ya picha AFP

Shirika la habari la taifa lilimnukuu Bwana Saleh akisema msamaha huo ni kwa wote waliofanya makosa wakati wa ghasia za Yemen, isipokuwa wale waliohusika na jaribio la kumuuwa yeye.

Msemaji wa upinzani amelitoa maanani tamko hilo.

Alisema kufuatana na mkataba uliotiwa saini juma lilopita wa kumvua madaraka Bwana Saleh, kiongozi huyo amekabidhi madaraka kwa makamo rais wake, na sasa hana haki ya kufanya uamuzi huo.