Joseph Kabila ashinda urais tena DRC

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bw Joseph Kabila

Bw Joseph Kabila ametangazwa mshindi wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo muda mfupi uliopita.

Kulingana na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo Joseph Kabila ameshinda kwa asilimia 48.95, mpinzani wake mkuu Etienee Thisekedi akiwa na asilimia 32.33 na Vital Khemere naye akipata asilimia 7.74.

Matokeo hayo yalitarajiwa kutoka siku ya Jumanne lakini maafisa walisema matatizo ya kusambaza vifaa katika nchi hiyo kubwa ndio yalisababisha ucheleweshaji huo.

Wakati huo huo usalama umeimarishwa iwapo patatokea ghasia kufuatia madai ya udanganyifu.