Huwezi kusikiliza tena

Wasanii wa bongoflava watumbuiza

Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara, Watanzania kwa ujumla walijumuika kusherehekea siku hiyo, moja ikiwa kwa njia ya burudani kutoka kwa wasanii wa Bongoflava.

Profesa J, Diamond na Ali Kiba walikonga nyoyo za washabiki wao katika shughuli iliyofanyika mjini London, kwenye ukumbi wa The Pulse.

Shughuli hiyo iliandaliwa na KASSU Entertainment. Picha za video zimepigwa na Zuhura Yunus.