Muasisi wa sarafu ya Euro alaumu

Afisa aliyekuwa rais wa baraza kuu la Umoja wa Ulaya, na waasisi wa sarafu ya Euro, Jacques Delors, amesema kulitokea makosa baada ya kuanzisha sarafu ya Euro mwaka wa 1999. Amesema nchi zilizokuwa dhaifu kifedha, haziku-shughulikiwavya kutosha.

Jacques Delors, ni kati ya watu waliobuni sarafu ya Euro kwa nchi za Umoja wa Ulaya. Alikuwa afisa muhimu katika umoja wa Ulaya kwa mwongo mzima. Lakini anasema, mipango yake iliyotayarishwa kwa uangalifu mkubwa, haikufuatwa.

Viongozi wa kisiasa, walio-osimamia kuasisiwa kwa Euro, walidharau matatizo yaliyojitokeza, na waliziacha nchi zanachama kuvunja shuruti. Akihojiwa na gazeti moja la Uingereza, Bwana Delors amesema juhudi za viongozi wa sasa wa mataifa ya Ulaya, kurekibisha matatizo ni dhaifu na zimechelewa.

Matamshi yake yanakuja katika juma muhimu Ulaya. Jumatatu, kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel na Rais Sarkozy wa Ufaransa, watakutana kutoa pendekezo la pamoja, la kudhibiti bajeti za nchi za Euro, ingawa kuna tofauti kubwa kati ya viongozi hao wawili.

Na mwisho wa juma, viongozi wote wa Umoja wa Ulaya, watakutana kutafuta ufumbuzi, katika mkutano wa kilele mjini Brussels ...mkutano wa vidole machoni.