Mapigano yaendelea Yemen

Mapambano yanaendelea katika mji wa Taez, wa pili kwa ukubwa nchini Yemen, baina ya jeshi la serikali na wapiganaji wa upinzani na wa makabila fulani; na kuzusha wasiwasi ikiwa makuabliano ya kumaliza ghasia za miezi kadha, yatatekelezwa.

Wafanyakazi wa hospitali mjini Taez, wameiambia BBC, kwamba watu saba zaidi wameuwawa na kufanya jumla ya vifo kuwa 30 tangu Alkhamisi.

Kati ya waliokufa watatu ni raia, na wengine ni wanajeshi na wapiganaji wa upinzani.

Mapigano hayo ni tishio kwa shughuli za kukabidhi madaraka kwa uongozi mpya, baada ya makubaliano yaliyotiwa saini na Rais Saleh mwezi uliopita.