Iran yadungua ndege ya Marekani

Jeshi la Iran linasema kuwa limedungua ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani, mashariki mwa nchi; na italipiza kisasi endapo ndege nyengine itaingia katika anga ya Iran.

Haki miliki ya picha Fars

Limesema kuwa ndege hiyo ni ya kufanya uchunguzi, na kwamba imetekwa bila ya kuharibika.

Wameitaja ndege hiyo kuwa ya aina ya RQ-170 Sentinel - ni ndege inayohepa radar, na Marekani ilikiri ikiunda ndege hiyo kwa siri miaka miwili tu iliyopita.

Jeshi la Iran limesema ikiwa Iran itaingiliwa tena, basi litajibu, na halitobaki ndani ya mipaka ya Iran tu.