Wanasayansi wavumbua chanjo ya Ebola

Haki miliki ya picha online
Image caption Virusi vya Ebola, wanasayansi wagundua chanjo

Wanasayansi wamevumbua chanjo inayowalinda panya dhidi ya aina hatari ya virusi vya homa ya Ebola.

Ebola ilitambulika mara ya kwanza mwaka 1976 wakati homa hiyo ilipoua zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa.

Watafiti wanasema hii ni chanjo ya kwanza kabisa ambayo inaweza kutumika kwa muda mrefu na kwa hiyo inaweza kuhifadhiwa bila ya matatizo yoyote.

Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la chuo kikuu cha Taifa cha kisayansi cha taifa nchini Uingereza.

Ebola huambukiza kupitia majimaji mwilini na inaweza pia kusambazwa kwa njia ya hewa. Wanaoathirika kawaida husikia kizunguzungu,kutapika,kuvuja damu na viungo kushindwa kufanya kazi kabla ya kufa.

Ingawa ni watu wachache sana wanaoambukizwa Ebola kila mwaka, athari zake huonekana na za kuangamiza kwa haraka sana.

Aghalabu kuna hofu kwamba unaweza kutumiwa katika vitendo vya ugaidi dhidi ya binadamu.

Inaelekea kuwa ni chanjo inayohifadhiwa kwa muda mrefu inajenga nguvu za kuangamiza kirusi cha Ebola. Chanjo hii mpya ina protini maalum ambayo inarahisisha kutambuliwa kirusi cha Ebola na ina nguvu zaidi inapohifadhiwa kwa muda mrefu.

Chanjo hii inahifadhi asilimia 80 ya panya wanaodungwa aina ya kirusi cha ebola inayoua, kwa mujibu wa daktari charles Armtzen wa chuo kikuu cha Arizona aliyehusika na utafiti huo.

Alisema hatua ijayo ni kuifanyia majaribio chanjo hii kwa kirusi cha Ebola ambacho kinakaribiana na kile kinachowaambukiza binaadamu.