Waingereza wapungukiwa imani

Utafiti wa mwaka uliofanyika hivi karibuni nchini Uingereza kuhusu mitazamo ya kijamii unaonyesha kua imani za watu masikini na wale waliokosa ajira zimezidi kupungua.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Uchumi watikiswa

Robo ya watu hao wamesema wandhani umaskini ni matokeo ya uvivu na ukosefu wa dhamira, wakati zaidi ya nusu wanaamini kiasi cha msaada unaopewa wasio na ajira ni kikubwa mno.

Utafiti pia unatoa mwangaza wa kuhusu fikra za Waingereza wakati huu ambapo uchumi unazidi kufanya maisha kua magumu baada ya miaka kadhaa ya uchumi ulionawiri na serikali kuzitumia fedha kwa namna ya kupindukia.

Image caption Kupungua kutegemea serikali

Kwa upande mmoja utafiti huo unaonesha kuwa kuna mabadiliko ya mitazamo, na Waingereza wengi hawataki kulipa kodi kubwa kwa ajili ya huduma za serikali huku wengine wakiilaumu serikali kwa hali zao kudhoofika na ukosefu wa ajira. Utafiti huo unahitimisha kwa kuonyesha sura inayoleta dhana kwamba msisitizo uliopo ni wa kila mmoja kuondokana na ile dhana ya dola kumtekelezea na badala yake kujiwajibisha. Bila shaka yoyote wanasiasa wa vyama vyote watakua na hamu ya kujifunza matokeo ya utafiti huo kwa kina.