Mabomu yalipuka kaskazini mwa Kenya

Mashambulio mawili ya mabomu yaliyofanywa kaskazini-mashariki mwa Kenya, karibu na mpaka wa Somalia, yameuwa askari mmoja wa Kenya na kuwajeruhi wengine kama 10.

Haki miliki ya picha internet

Miripuko hiyo iliyotokea karibu na miji ya Mandera na Wajir, yaliwalenga askari waliokuwa wakipiga duru na msafara wa jeshi.

Mashambulio kadha yamefanywa nchini Kenya, tangu ilipotuma wanajeshi wake huko Somalia, kuwasaka wapiganaji wa Kiislamu wa kikundi cha al-Shabaab miezi miwili iliyopita.