Iran yafanya mazoezi ya jeshi

Jeshi la wanamaji la Iran linafanya mazoezi kadha karibu na Hormuz mlango wa kuingilia Ghuba, moja kati ya njia zinazotumiwa sana na meli za mafuta.

Haki miliki ya picha AFP

Mkuu wa jeshi la wanamaji la Iran, Habibollah Sayyari, alisema mazoezi hayo ya siku kumi yamekusudiwa kuonesha nguvu za nchi hiyo za kujihami na kujikinga.

Alisema mazoezi yatatoa nafasi ya kujaribu makombora mepya, makombora ya baharini na silaha nyengine.

Taarifa zisizothibitishwa za juma lilopita, kwamba Iran ikipanga kufunga njia ya baharini ya Hormuz, zilipelekea bei ya mafuta kupanda kwa muda mfupi.