Libya yasherehekea siku ya uhuru

Kwa mara ya kwanza katika miongo mine, Libya inasherehekea siku iliyopata uhuru kutoka kwa Utaliana miaka 60 iliyopita.

Haki miliki ya picha AFP

Wakati wa utawala wa Kanali Gaddafi, WaLibya wakiruhusiwa kusherehekea tu siku aliyonyakua madaraka mwaka wa 1969.

Katika sherehe za leo kunafanywa mhadhara kutoka medani ya mashujaa, kati ya mji mkuu, Tripoli, hadi kasri ya zamani ya mfalme.