Mapigano ya Nigeria yauwa 50

Inaarifiwa kuwa mpambano kaskazini mwa Nigeria baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa Kiislamu, yameuwa watu kama 50.

Haki miliki ya picha google

Mkuu wa jeshi, alisema wanajeshi watatu walikufa na wengine saba kujeruhiwa, kwenye mapambano katika mji wa Damaturu hapo jana.

Jeshi limeuwa zaidi ya wapiganaji 50 wa kikundi cha Boko Haram.

Mtu aliyeshuhudia matukio hayo aliiambia BBC kwamba risasi na miripuko ya mabomu yaliwafanya watu wengi waukimbie mji wa Damaturu.

Maiti za watu 46 zinaarifiwa kupelekwa chumba cha maiti mjini Damaturu na mji wa jirani, Maiduguri.