Wanawake watengwa kwenye basi Israel

Waisrail wanazozana kuhusu kuwatenga wanawake Haki miliki ya picha Getty

Mamia ya Wayahudi wanaofuata dini yao kiasilia, wamepambana na polisi karibu na Jerusalem kwa sababu ya mvutano kuhusu kuwatenga wanawake na wanaume.

Afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa katika mji wa Beit Shamesh, wakati polisi walipoitwa kuondoa ilani kwenye barabara kuu, inayoamrisha wanawake wajitenge na wanaume.

Makundi ya Wayahudi wanaofuata dini yao kiasili waliwafukuza polisi na kuwarushia mawe.

Ghasia hizo ndio za karibuni kabisa katika mfululizo wa matukio mengine nchini Israil, ambapo wanawake walilazimishwa kukaa nyuma kwenye mabasi, katika maeneo ya Wayahudi hao, ingawa mahakama yametoa amri kuwa wanaweza kukaa watakapo.