Marehemu wakumbukwa Nigeria

Nigeria, kanisa liloshambuliwa Haki miliki ya picha Reuters

Mamia ya watu wamehudhuria sala ya kuwakumbuka marehemu nchini Nigeria kwenye kanisa la Wakatoliki, ambamo watu zaidi ya 30 waliuwawa katika shambulio la mabomu Jumapili.

Shambulio hilo nje ya mji mkuu, Abuja, lilikuwa la mwanzo katika mashambulio kadha siku ya Krismasi yaliyofanywa dhidi ya makanisa na majengo ya polisi.

Watu zaidi ya 40 walikufa.

Kikundi cha Kiislamu cha Boko Haram, kimesema kuwa kilifanya mashambulio hayo.

Kiongozi mkuu wa upinzani, Muhammadu Buhari, ameishutumu serikali kuwa imechelewa kuanza kushughulikia mashambulio hayo; na alisema Rais Goodluck Jonathan hakusema kitu, hadi mashambulio hayo kuanza kulaaniwa dunia nzima.