Guruneti lauwa watoto Kenya

Wanajeshi wa Kenya Haki miliki ya picha AFP

Watoto watatu wameuwawa nchini Kenya na lile linaloshukiwa kuwa ni guruneti liloripuka walipokuwa wanalichezea.

Polisi katika jimbo la magharibi la Mount Elgon, walisema inaelekea guruneti hilo liliachwa wakati wa mapigano baina ya jeshi na wapiganaji wa eneo hilo, katika mzozo kuhusu ardhi, mwaka wa 2008.

Jeshi lilisema, guruneti hilo siyo la aina wanayo-tumia.