Wengi wanasurika katika boti Lamu

Watu karibu 16 wanahofiwa kufa katika ajali ya mashua iliyozama Lamu, Kenya, Jumapili usiku.

Haki miliki ya picha AFP

Hadi sasa watu kama 50 wameokolewa au kujinusuru wenyewe kwa kuogelea. Inahofiwa kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba abiria kama 70, ingawa inafikiriwa kuwa ilikuwa imesheheni abiria zaidi ya ile idadi inayoruhusiwa.

Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa miili 7 imepatikana.

Watu kadha wametoweka, lakini inaarifiwa waokozi hawajakuta miili katika mashua iliyozama

Joseph Sigei ambaye ni naibu wa afisa mkuu wa polisi katika eneo la Lamu Magharibi aliiambia BBC kwamba hafikiri kama wale waliobaki majini kucha watakuwa hai.