Kenya yasema al-Shabaab yasambaratika

Jeshi la Kenya linasema kuwa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al-Shabaab, kinasambaratika, huku shambulio la Kenya nchini humo linamezidi kuwa na kasi.

Haki miliki ya picha internet

Msemaji wa jeshi la Kenya, Kanali Cyrus Oguna, aliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi, kwamba mgawanyiko kati ya viongozi wa al-Shabaab unamaanisha kuwa mwisho wa kikundi hicho hauko mbali.

Alisema mashambulio yaliyofanywa na ndege za Kenya hapo jana yaliuwa wapiganaji wa al-Shabaab kama 60, na kwamba wapiganaji 20 wamejiunga na upande wa jeshi la Kenya, katika muda wa majuma mawili.

Lakini mwandishi wa BBC Afrika Mashariki, anasema ni shida sana kuthibitisha taarifa hizo.

Al-Shabaab inasema itawashinda Wakenya.