Ajali ya meli Utaliana yauwa watu watatu

Waokozi wa Utaliana wanakagua meli iliyopinduka upande mmoja baada ya kwenda mrama nje ya pwani ya magharibi Ijumaa usiku na kuuwa watu kama watatu.

Abiria wanasema walisikia kishindo kikubwa kabla ya meli hiyo, Costa Concordia, kutikisika na kusimama na taa kuzimika.

Mlinzi mmoja wa pwani alisema baadae kwamba meli hiyo iligonga kitu - ambacho kilipasua meli upande wa kushoto.

Meli ilipoanza kuingia maji, kilipigwa king'ora kuwaonya watu watoke kwenye meli, na abiria na mabaharia zaidi ya 4000 walichupa majini na kuogelea hadi kisiwa cha Giglio kilioko karibu na eneo la ajali.