Mapinduzi ya Tunisia yatimiza mwaka

Rais wa Tunisia, Moncef Marzouki, ametumia fursa ya sherehe za kuadhimisha mwaka tangu serikali ya kidikteta kupinduliwa, kuwahakikishia Watunisia kwamba kujitolea mhanga kwao mwaka uliopita, hakutakuwa ni bure tu.

Haki miliki ya picha Reuters

Katika hotuba iliyotangazwa taifa zima, Rais Marzouki alisema mapinduzi ya Tunisia, ambayo yalipelekea mwamko wa nchi za Kiarabu katika Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati, yalifungua mlango wa kuleta hatima njema.

Lakini katikati ya mji wa Tunis, maelfu ya watu waliandamana kulalamika juu ya hali ya nchi.

Waandishi wa habari wanasema Tunisia inakabili ukosefu wa ajira unaozidi, machafuka ya kijamii, na rushwa inaendelea.