Maiti mbili zapatikana melini Utaliana

Mlinzi wa pwani katika kisiwa cha Giglio, Utaliana, anasema maiti za wanaume wawili wazee zimekutikana katika upande uliozama wa meli ya abiria iliyokwenda mrama, Costa Concordia.

Haki miliki ya picha AP

Idadi ya watu waliokufa imefikia watano, tangu meli hiyo kufikwa na ajali Ijumaa usiku.

Watu wengine kadha wametoweka.

Nahodha wa meli anahojiwa, kujaribu kujua chanzo cha ajali.

Aliiambia televisheni ya Utaliana kwamba, kufuatana na ramani zake, meli ilikuwa mbali vya kutosha na ufukwe, na isingetarajiwa kugonga mwamba.

Hapo awali, afisa mmoja wa meli hiyo aliyejeruhiwa, aliokolewa na kupelekwa hospitali.