Msamaha kwa wafungwa wa kisiasa Syria

Rais Bashar al- Assad wa Syria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Bashar al- Assad wa Syria

Wachunguzi wa muungano wa nchi za Kiarabu walioko nchini Syria wameonyeshwa kundi la wafungwa walioachiliwa huru.

Kulingana na maafisa nchini humo kundi hili la wafungwa ni sehemu ya kile wametaja kama msamaha wa jumla wa uhalifu uliotekelezwa wakati wa machafuko ya miezi kumi dhidi ya rais Bashar al- Assad.

Syria imekubali mpango wa muungano wa nchi za kiarabu ambao unajumisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa.

Lakini mwandishi wa BBC mjini Damascus amesema baadhi ya walioachiliwa walimueleza kuwa hawakuhusika na machafuko yanayoshuhudiwa.

onyo kwa rais Assad

Awali, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon, amerudia wito wake wa kutaka maafisa nchini Syria kuacha kuuwa watu wake.

Akizungumza nchini Lebanoni, Bwana Ban amesema mapinduzi katika nchi za Kiarabu yamenyesha kuwa watu hawataendelea kukuabali uongozi wa kidikteta.