Watalii watekwa na kuuawa Ethiopia

Haki miliki ya picha
Image caption Eneo la Afar maarufu kwa volkano nchini Ethiopia, watalii wametekwa na kuuawa

Takriban watu wanne wametekwa nyara na watalii wa kigeni watano wameuawa katika shambulio karibu na mpaka wa Ethiopia na Eritrea, serikali ya Ethiopia imesema.

Watalii hao watano wa kigeni wameuawa katika shambulio kutoka kwa watu wenye silaha wasiojulikana kaskazini mwa eneo la Afar , serikali imesema.

Raia wa Ujerumani, Ubelgiji, Italia na Hungary walikuwa ni miongoni mwa mwao, afisa wa serikali Bereket Simon alisema.

Wazungu wawili ilisemekana kuwa walitekwa nyara katika shambulio hilo pamoja na polisi mmoja na dereva.

Eritrea imekanusha vikali tuhuma za serikali ya Ethiopia kwamba iliwasaidia watu hao wenye silaha.

Eneo la vijijini la Afar linachukuliwa kuwa ni la shida kwa waasi wa Ethiopia na Eritrea.

Ethiopia na Eritrea wamekuwa mahasimu wakubwa tangu vita vyao kuhusu mpaka kati ya mwaka 1998-2000.

Watalii hao inaaminika kuwa walikuwa wanalitembelea eneo hilo la volkano la Afar ambalo waandishi wa habari wanasema lina joto kali na halina usalama wakati waliposhambuliwa Jumatatu.

Raia wa Ulaya watano waliuawa.Wawili walijeruhuwa vibaya na watatu alitoroka bila kujeruhiwa, Televisheniya Ethiopia (ETV) iliripoti.

Watalii wawili waliojeruhiwa wamepelekwa katika zahanati ya jeshi, ilisema.

'Wamechukuliwa mpakani'

Wanne hao walitekwa katika mpaka wa Eritrea, Bw Bereket alisema.

Aliwashutumu watu hao wenye silaha kwa shambulio hilo ambao alisema ‘walipewa mafunzo na silaha na serikali ya Eritrea.’

"Kwa tukio la kawaida la kigaidi na utawala,’ aliliambia shirika la habari la Reuters.

Lakini madai kama hayo yalikuwa ‘ni uongo mtupu,’ balozi wa Eritrea katika Umoja wa Afrika, Girma Asmerom, aliliambia shirika la habari la Associated Press.

Waandishi wanasema Ethiopia mara kwa mara imekuwa ikituhumu Eritrea kwa kuwaunga mkono waasi.

Eritrea ilipata uhuru kutoka Ethiopia mwaka 1993 lakini nchi hizo mbili muda mfupi tu zikawa na mzozo wa mpaka.

Mwaka 2007, raia wa Ulaya watano na wa Ethiopia 13 walitekwa katika eneo la Afar. Ethiopia inaituhumu Eritrea kwa kuhusika na utekaji nyara huo ingawa Eritrea inawalaumu waasi wa Ethiopia.

Mateka hao baadaye waliachiliwa huru.

Kuna hatari kuwa tukio hilo linaweza kuchochea zaidi uhasama kati ya mataifa hayo mawili ambayo tayari ni maadui wakubwa, mwandishi wa BBC Afrika Mashariki Will Ross anasema.