Besigye akamatwa Uganda

Besigye Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Besigye akamatwa tena na mamlaka za Uganda

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye na wanasiasa wengine wamekamatwa muda mfupi kabla ya kuhudhuria mkutano wa hadhara mjini Kampala.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala, Joshua Mmali amesema polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi hilo la wanasiasa, kabla ya kuwapeleka katika kituo cha polisi.

Bw Besigye alikamatwa mara kadhaa wakati wa mapambano kati ya wafuasi wake na majeshi ya usalama.

Walikuwa wakipinga kile wanachodai kuvurugwa kwa uchaguzi mwezi Februari mwaka 2011, na kupanda kwa gharama za maisha.

Mwandishi wetu alisema mapema kuwa polisi walipelekwa katika nyumba za wanaisasa maarufu ili kuwazuia kuondoka majumbani mwao.

Polisi bado hawajasema kwa nini Bw Besigye na wengine wanashikiliwa.

Upande wa upinzani unadai kuwa serikali ya Rais Museveni "imeshindwa na sera za kiuchumi" na kusababisha gharama za maisha kupanda kupita kiasi nchini Uganda.