Eritrea yadaiwa kuhusika na mauaji

Watalii waliotoweka nchini Ethiopia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watalii waliotoweka nchini Ethiopia

Ethiopia imelaumu taifa jirani la Eritrea kwa kuwaua na kuwateka nyara watalii kutoka Ulaya katika eneo la mpaka kati ya mataifa hayo mawili.

Watalii watano waliuawa na Wajerumani wawili na Waethiopia wawili katika shambulio hilo la Jumatatu.

Serikali ya Ethiopia imesema hiyo si mara ya kwanza kwa Eiritrea kutekeleza visa vya ugaidi dhidi ya watalii wanaotembelea Ethiopia.

Lakini Eritrea imekanusha kuhusika na tukio hilo.

Mwakilishi wake katika Muungano wa Afrika, Girma Asmeron, ametaja madai hayo kama "uongo mtupu."

Mataifa hayo mawili yalipigana katika mzozo wa mpaka kati ya mwaka 1998 na mwaka 2000.