Goodluck aahidi kuwashinda magaidi

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ameahidi kuwa atawashinda watu waliofanya mashambulio katika mji wa Kano, kaskazini mwa nchi, na ambayo yaliuwa watu zaidi ya 150.

Haki miliki ya picha AP

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kwanza katika mji huo tangu mashambulio ya Ijumaa, Bwana Jonathan alisema mashambulio hayo yalikuwa dhidi ya Wanigeria wote.

Chama cha wapiganaji wa Kiislamu cha Boko Haram, kilisema kilihusika na mashambulio hayo.

Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amelaani utumiaji nguvu huo, na alisema anashutushwa kuwa inatokea mara nyingi, na ukubwa wake.