Ghasia zaendelea Nigeria

Watu kama wanane inaarifiwa kuwa wamekufa katika mashambulio mengine kaskazini mwa Nigeria.

Haki miliki ya picha 1

Katika mji wa Tafawa Balewa kwenye jimbo la Bauchi, kituo cha polisi kilishambuliwa na mapambano ya risasi yalitokea baina ya polisi na watu waliokuwa na bunduki.

Inaarifiwa kuwa mwanajeshi mmoja aliuwawa kwenye kituo cha ukaguzi katika eneo jengine.

Makamo wa rais wa Nigeria, Namadi Sambo, yuko njiani kuelekea mji wa Kano, ambako watu kama 100 waliuwawa kwenye miripuko kadha ya mabomu Ijumaa usiku.

Chama cha wapiganaji wa Kiislamu cha Boko Haram kilidai kuhusika na mashambulio ya mjini Kano.